Makonda ateta na viongozi wa dini

 GEITA: Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda amewashukuru na kuwaomba viongozi wote wa dini nchini, kudumisha ushirikiano kwa viongozi wa chama na Serikali, kwa kushauri na kutoa miongozo itakayowasaidia kuendelea kuwatumikia watanzania kwa haki na ufanisi ili kugusa matumaini yao kwenye nyanja mbalimbali za maendeleo nchini.



Makonda amesema hayo alipokwenda kumuona na kumsalimia Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita, Mhashamu Baba Askofu Flavian Matindi Kassala, ofisini kwake, jimboni, mtaa wa Kambarage 14, mjini Geita, Desemba 28, 2023.


Huo ni mwendelezo wa utaratibu wake wa kwenda kuwaomba ushirikiano, ushauri na miongozo mbalimbali viongozi wa kiroho wa madhehebu ya dini mbalimbali nchini, pamoja na makundi mengine ya kijamii, utakaomsaidia katika utekelezaji wa majukumu yake.


Kwa upande wake, Mhashamu Baba Askofu Kassala, pamoja na kumtakia kila la heri, amemhakikishia Makonda kuwa viongozi wa dini wataendelea kutoa ushirikiano wao katika kuiombea nchi, kuwashauri viongozi na kuwapatia miongozo mbalimbali.


Aidha, kwa pamoja wamefanya maombi ya kuliombea taifa.


Huu ni muendelezo wa ziara za Makonda katika kuwatembelea viongozi mbalimbali wa dini nchini.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE