YANGA YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA POLISI TANZANIA


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa kesh, Oktoba 22, Uwanja wa Uhuru dhidi ya Polisi Tanzania.


Mchezo huo ni wa raundi ya sita kwa Yanga unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na rekodi za timu hizi mbili kwa msimu uliopita wa 2019/20.

Kwenye mechi mbili ambazo walikuwa wanasaka pointi sita kila timu iliambulia pointi mbili kwa kuwa mechi zote mbili ngoma ilikuwa ni sare.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Yanga ililazimisha sare ya kufungana mabao 3-3 na ule wa pili uliochezwa Uwanja wa Ushirika, Moshi, Polisi Tanzania ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi.

"Kila kitu kinakwenda sawa, mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu yao kwa kuwa maandalizi yapo vizuri.


"Ushindani utakuwa mkubwa lakini nasi tumejipanga kuona namna gani tutapata ushindi kwenye mchezo wetu," amesema.


Yanga kwenye msimamo ipo nafasi ya tatu ikiwa imecheza mechi tano na pointi zake ni 13, Polisi Tanzania ipo nafasi ya tano ikiwa imecheza mechi sita na ina pointi 11.


Ikiwa imecheza mechi tano ilishinda mechi nne ikiwa ni ile dhidi ya Mbeya City, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar ambapo ushindi wake ulikuwa ni wa bao 1-0 na ile dhidi ya Coastal Union ilishinda kwa mabao 3-0.


Sare moja ilikuwa ni ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons na mfungaji akiwa ni Michael Sarpong.



0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE