SIMBA: TUNATAKA KUFIKA MBALI KIMATAIFA

 


BEKI wa kati wa Simba, Pascal Wawa amesema kuwa hesabu kubwa za timu hiyo ni kuweza kufika mbali kimataifa jambo litakalowafanya wapambane kwenye mechi yao dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe.

Tayari kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck kipo nchini Zimbabwe ambapo kiliwasili Desemba 18 na orodha ya wachezaji 24.

Wawa raia wa Ivory Coast ni miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye orodha hiyo ambayo imeanza kujiweka fiti.

 Kazi yao ya kwanza raundi watapambana Desemba 23 mbele ya FC Platinum ambapo ameweka wazi kwamba wataingia uwanjani kupambana ili kupata matokeo chanya.


"Tutahakikisha tunapambana kufanya vizuri kwenye mchezo wetu kwa kuwa malengo yetu ni kuona kwamba timu inafika mbali kimataifa.

"Ili kufika huko hatuna namna ni lazima tupambane kupata matokeo chanya ndani ya uwanja hivyo mashabiki wazidi kutuombea dua," .



0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE