KUMBE! SIMBA WANAAMINI KWAMBA TAREHE 8 HAWATOKI MBELE YA YANGA


IKIWA inaelekea Kariakoo Dabi, Mei 8, 2021 kati ya Simba na Yanga, kauli ya Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara aliyotoa kuhusu tarehe 8 anaamini kwamba hawatoki.

Hiyo aliiweka wazi alipokuwa akifanya mahojiano na Azam TV kuhusu mechi ya Simba v Yanga ambayo ilichezwa Julai 12 kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho ambapo Simba ilishinda kwa mabao 4-1.

Mahojiano haya yalifanyika Julai 8 kwenye kipindi cha WednesdayNightLive.

Manara alisema namna hii:" Always, (mara nyingi) watu hawajui historia, namba 12 inafiti kwa Simba, ninawaonea huruma, yaani wale bora ingebaki tarehe 11 walipobadili kusema itakuwa tarehe 12 nikasema ooh, sisi tunaamini katika takwimu na namba kama hizi.

"Na tarehe 8/18, Charles Hilal Mkwangwa ataikumbuka hii alikuwa mtangazaji, radio Tanzania alisema ni yuleyule wa Mei 18, Said Sued Scadi anaipatia tena Yanga goli,yaani 8,muulize Mkwanga hii clip, alitumia neno ni yuleyule mwaka 1991 miaka 29 nyuma alitangaza hivyo, mara ya pili.

"Yaani ikishafika tarehe 8,18,28 sisi hatutoki na sisi ikija tarehe 2,12,22 hawatoki. Mimi mswahili, siamini kwamba uchawi ingawa upo lakini kwenye mambo haya vilele, utakosaje kuamini.

"Mimi ile tarehe 8 nilipoamka asubuhi nilikuwa na Hashim Ibwe nilimwambia kwamba tunafungwa, aliponiuliza kwa nini nilimwambia kwamba nimeamka nimemuona mtu kaja mlangoni kanisalimia kisharishari, wewe huwezi kumuona hauna maarifa hayo.

"Wakati mechi inachezwa Diamond alinipigia simu akasema mimi ninatua Paris unakuja lini? Nikamwambia mimi kesho, unajua hapa tunacheza  na tumefungwa goli moja? Akasema bado dakika ngapi? Nikwambia bado dakika 10 akasema litarudi ila nikamwambia kwamba halirudi na tukifanya mchezo tutaongezwa bao la pili.

"Sprit ya wachezaji wa Yanga waliyokuwa nayo, walijitoa asilimia 100, ninadhani kwamba wachezaji wa Simba wananiskia na watafanya hivyo, watajituma,".

Katika mchezo wa Yanga v Simba uliochezwa Machi 8, ubao ulisoma Yanga 1-0 Simba na ni Bernard Morrison alipachika bao hilo la ushindi kwa Yanga ila kwa sasa yupo Simba.

Safari hii Uwanja wa Mkapa, Mei 8 itakuwa ni Simba v Yanga, ni suala la kusubiri na kuona je namba 8 itakuwa upande wa Yanga ama itakuaje.



0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE