Polisi watoa kauli mvua zinazoendelea kunyesha

 


Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, David Misime Amewataka Wananchi kuchukua tahadhari kubwa wanapotaka kuvuka mito,madaraja,makorongo ambayo yamejazwa na mvua zinazoendelea kunyesha ambapo ameongeza kuwa mvua zinazoendelea kunyesha hazina urafiki na yeyote anayetakakushindana nazo.


Misime amesema tayari wamepokea taarifa mbalimbali za watu wazima na watoto kufa maji wakati wakijaribu kuvuka mito na barabara zilizojaa maji na wengine wakiogelea kwenye mashimo, madimbwi Pamoja na mabwawa yaliyojaa maji ya mvua.


Aidha, amewaomba wazazi na walezi kuongeza ungalizi Mkubwa kwa watoto kipindi hiki cha mvua ambazo zimetabiriwa kuendelea kunyesha maeneo mbalimbali ya nchi na amewataka wazazi kuwaonya na kutowaruhusu kwenda kucheza au kuogelea kwenye mito.


Misime pia amewasihi Wananchi wote ambao wamechimba mashimo na kuyaacha wazi wayafukie ili yasihatarishe Maisha ya watu, huku akitoa wito kwa Viongozi wa Serikali za Mitaa kuendelea kushirikiana na Polisi Kata, kutoa elimu na tahadhari kwa wananchi ili kuwaepusha madhara ya mvua zinazoendelea kunyesha.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE