Mtambo wa matibabu wa kwanza A.Mashariki wazinduliwa Muhimbili

 


DAR ES SALAAM: HOSPITALI ya Taifa Muhimbili leo imezindua mtambo wa Hyperbaric Medicine unaotibu magonjwa mbalimbali kwa kutumia asilimia 100 ya hewa tiba mgandamizo ya oksijeni.


Mtambo ambao ni wa kwanza kwa Afrika Mashariki na wapili kwa Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.


Hayo yameelezwa na Mtaalamu wa Hyperbaric Medicine kutoka Muhimbili, Dk Albert Magohe na kusema kuwa mtambo huo unatibu magonjwa mengi ambayo hayakuwezekana kutibiwa nchini hapo awali.


“Mtambo huu husaidia matibabu ya magonjwa mbalimbali ikiwemo madonda sugu yatokanayo na kisukari, maambukizi ya kwenye mifupa, waliopata madhila ya matibabu ya mionzi, waliopoteza uwezo wa kusikia, walioungua kwa muda mrefu, wale wenye upotevu mkubwa wa damu na kutokana na hali zao hawatakiwi kuongezewa damu,


“Pia hutibu waliopata madhara ya bahari yanayoweza kupelekea kiharusi kwa mgonjwa ‘Decompression sickness’ kutokana na uvuvi au utalii wa kuzamia chini ya maji,” amesema Dk Magohe.


Amesema muda wa mgonjwa kupona hutegemea na ukubwa wa madhara aliyonayo mgonjwa.


“Kwa mfano wale waliodhurika na kuzamia majini wao ‘sessions mbili’ awamu mbili za matibabu ya dakika 90 yanaweza kumsaidia.” Ameelezea mtaalamu huyo.


Akizungumzia gharama za mtambo huo Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Profesa Mohamed Janabi amesema mtambo huo umetengenezwa na Kampuni ya Sechristl na umegharimu Sh milioni 250.


Prof Janabi amesema mpaka sasa kuna wataalamu watano tu nchini ambao ni wauguzi watatu na madaktari wawili waliokuwa mafunzoni katika Chuo cha Marekani cha Dartmouth.


“Naomba kufikia mwakani, kupitia ninyi tupate manesi wengine watatu na madaktari wawili.” Amesema Profesa huyo.


Mkurugenzi huyo amesema kutokana na umuhimu wa mtambo huo wamataraji kununua mitambo mingine ili kuwahudumia wagonjwa zaidi.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE