Msiingize vidole ukeni, mtapata saratani – Zuhura

 


DAR ES SALAAM: KUNAWA kwa kuingiza vidole sehemu za uke, kujifukiza na matumizi ya bidhaa mbali mbali ikiwemo asali kuwekwa ukeni, wapenzi wengi, kujamiiana katika umri mdogo, maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) kumetajwa kusababisha ongezeko kubwa la saratani ya kizazi.


Tafiti zinaonesha kuwa wale wanaojisafisha sehemu za uke kwa kujiingiza vidole wako hatarini kwa sababu huwa wanaondoa bakteria walinzi waliopo ukeni. Ukiwaondoa hao bakteria, virusi wanaweza kujibadilisha na kuwa saratani.


Akizungumza na HabariLeo, Mratibu wa Kitaifa wa Afya ya Mama na Mtoto, Zuhura Mbuguni amesema uke unajisafisha wenyewe kuingiza vitu tofauti ni hatari kwa mwanamke.


“Uke unajisafisha wenyewe, kuingiza kitu kisicho cha kawaida kinaharibu bakteria wake wa asili, kuna wanawake wengine wanatabia ya kujiwekea vitu vyenye kemikali kama sabuni mara wengine wanaweka asali, ndimu, perfyume, kujifukuza ili kuwaridhisha wanaume, vitu hivi vinaua wale bakteria walioko sehemu za uke na vingine husababisha mchubuko, hivi vyote ni hatari kwa mwanamke,”amesema Zuhura


Amesema, mbali na saratani ya kizazi, madhara mengine wanayoweza kupata wanawake wanaotumia vitu hivyo ni ugumba, kuziba kwa mirija ya uzazi, shambulizi ukeni, maumivu makali chini ya tumbo na maumivu wakati wa kujamiiana.


Kwa mujibu wa takwimu za Tanzania demographic health survey (TDHS) 2023 zinaonyesha saratani ya shingo ya kizazi bado inaongoza nchi na kuwa tishio ikiongoza kwa asilimia 34.3 ya saratani zote.


Kwa mujibu wa takwimu hizo zinaonyeshaka kuwa wanawake milioni 18.8 Tanzania, wenye umri wa miaka 15 hadi 44 na kuendelea wapo kwenye hatari ya kuapta saratani ya shingo ya kizazi.


Kwa mujibu wa takwimu hizo kati ya wanawake 10241 waliopimwa, wanawake 6525 walipoteza maisha.


Afrika Mashariki ina idadi kubwa zaidi ya vifo vinavyohusiana na saratani ya shingo ya kizazi duniani kote, kati ya wanawake 100,000 asilimia 42.7 wana maambukizi ya saratani ya kizazi, Tanzania ikishika nafasi ya pili baada ya Kenya.


Kwa upande wa Waziri Ummy Mwalimu alikaririwa akisema kuwa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha kuwa kila mwaka Tanzania ina wagonjwa wapya wa Saratani 42,000 ambapo wagonjwa hao wapya wanaofika kwenye vituo vya huduma za afya ni takribani 15,900 tu.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE