Mbeya kuanza kupima virusi vya ukimwi kwa ATM

 Mkoa wa Mbeya umefunga ATM maalum kwa ajili ya wananchi kujipima VVU wenyewe kwa hiyari, ili kudhibiti maambukizi mapya ya Virusi Vya UKIMWI (VVU).



Mradi huo wa mashine za ATM zinazotoa vipimo vya UKIMWI na kinga unatekelezwa na mfuko wa dharura wa Rais wa Marekani PEPFA na kutekelezwa na shirika la HJFMRI katika mikoa ya nyanda za juu kusini.


Kwa mujibu wa takwimu hizo za TACAIDS asilimia saba ya watu wazima Tanzania wenye umri wa miaka 15-49 wameambukizwa Virusi vya UKIMWI ambapo maambukizi kwa wanawake ni juu zaidi asilimia nane kuliko ya wanaume wenye asilimia sita.


Mikoa inayoongoza kwa maambukizi makubwa ya UKIMWI Tanzania ni Mbeya asilimia 14, Iringa asilimia 13 na Dar es Salaam asilimia 11.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE