Fahamu Kwa Undani Ugonjwa Wa Tetanus (Pepopunda).

 Mada yetu ya leo itauchambua ugonjwa huu wa tetanus ili uweze kujua chanzo cha tetanus, dalili zake, tiba au kinga ya tetanus. Bila kupoteza muda, tuanze mara moja.



》Tetanus Ni Nini?


Tetanus ni ugonjwa mkali, ambao mara nyingi unaua, ni wa mfumo wa neva unaosababishwa na sumu zinazotengenezwa na bakteria aitwaye (Clostridium tetani).

💉 Bakteria huyu hupatikana kwenye udongo na kwenye utumbo wa binadamu na wanyama (kinyesi). 💉 Bakteria huyu anaweza kuwa kimya kwa miaka mingi kama (spore) kabla ya kuzinduka na kugeuka bakteria anayezaliana. 💉 Bakteria huyu huzaliana kwenye kidonda. Vidonda vyenye kina au vile vyenye tishu zilizokufa ndiyo maeneo ambayo bakteria huyu anaweza kuingilia kirahisi mwilini. 💉 Sumu kali (tetanospasmin) inayozalishwa wakati bakteria hawa wanazaliana ndicho chanzo cha madhara makubwa ya tetanus. 💉 Sumu za tetanus huharibu mawasiliano baina ya neva na misuli inayoamshwa na neva hizo, na hasa sehemu vinapokutana (neuromuscular junction). 💉 Sumu za tetanus hukuza ishara za kikemikali kutoka kwenye neva kwenda kwenye misuli, hali inayosababisha misuli kukaza moja kwa moja.


🎯 Dalili Za Tetanus. Tetanus huchukua muda wa wastani wa kati ya siku 2 hadi miezi miezi 2 kuanza kuonyesha dalili zake, lakini kwa kawaida ni katika siku 14 toka siku ya kupata jeraha 👉🏿 Homa, Kupanda kwa pressure, Mapigo ya moyo kwenda mbio. 👉🏿 Kukaza kwa misuli kwenye taya (trimus) 👉🏿 Ugumu wa misuli ya shingo, 👉🏿 Shida wakati wa kumeza, 👉🏿 Ugumu wa misuli ya tumbo, 👉🏿 Mikazo ya misuli inayodumu kwa dakika kadhaa, mikazo ambayo inasababishwa na vitu vidogovidogo kama sauti kubwa, kuguswa au mwanga. 👉🏿 Katika siku saba za mwanzo baada ya maambukizi ya bakteria, kukaza kwa misuli kunakosababishwa na sumu za tetanus kwenye eneo la kidonda kutasambaa hadi sehemu nyingine zote za mwili. 👉🏿 Kukosa utulivu na maumivu ya kichwa vitaonekana. 👉🏿 Hii itahusisha misuli yote ya mwili ikiwa ni pamoja na misuli muhimu inayohusika na upumuaji. 👉🏿 Misuli hii ya upumuaji inapokosa nguvu, kupumua inakuwa ni shida au haiwezekani na kifo kinatokea endapo msaada wa kuokoa maisha utakosekana. 👉🏿 Pamoja na vifaa vya kusaidia upumuaji, maambukizi kwenye njia za hewa ndani ya mapafu yanaweza kusababisha kifo.


🎯 Kinga Ya Tetanus. 💉 Njia bora kabisa ya kupambana na tetanus ni kuizuia. Sumu za tetanus zikishanata kwenye maeneo zinapoishia neva, hakuna njia za kuziondoa. Ili kupona kutokana na sumu ya tetanus inabidi neva mpya ziote, tendo ambalo linachukua hadi miezi kadhaa. NB: Unaweza kujikinga na tetanus kirahisi sana kwa kutumia chanjo. Watoto wote wanatakiwa wapewe chanjo ya tetanus, kuanzia wanapokuwa na miezi 2 na kuimaliza wanapofikia miaka 5. Sindano za ziada (Booster vaccination) zinapendekezwa wanapofikia miaka 11 💉 Baadaye wanatakiwa kupata chanjo (follow-up booster vaccination) kila baada ya miaka 10.


🎯 Tiba Ya Tetanus "UGONJWA WA TETANUS HAUNA DAWA" 💉 Tiba hutolewa ili kuwaua bakteria kwa kutumia antibiotics wakati mgonjwa akichunguzwa juu ya dalili zo zote za kushindwa kupumua. 💉 Tiba inalenga kuzuia utengenezwaji wa sumu, kupunguza makali yake, na kudhibiti mikazo ya misuli. 💉 Hali ikiwa mbaya zaidi, mgonjwa atapewa vifaa vya kumsaidia kupumua. Sumu inayozunguka ndani ya mwili itaondolewa kwa kutumia antitoxin drugs. Sumu ya tetanus haisababishi madhara ya kudumu kwenye mfumo wa neva. NB: Baada ya kupona, mgonjwa bado atatakiwa kupata chanjo dhidi ya tetanus. Usijisahau Jalii afya yako, Kumbuka kwamba afya yako ndiyo mtaji wa maisha yako.


Makala hii imeandaliwa na mr health

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE