TMA yatabiri upepo mkali, wakazi maeneo ya pwani wapewa tahadhari


Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewataka wakazi wa mikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Tanga, Pwani pamoja na wale wa Visiwa vya Pemba na Unguja kuchukua tahadhari na kujikinga na upepo mkali kwa siku tano mfululizo.



Ushauri huo wa tahadhari umetolewa na leo Alhamisi ya Julai 13, 2023, huku ikitabiri kutokea upepo mkali usiozidi kilomita 40 na mawimbi makubwa yasiyozidi mita mbili kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa bahari ya Hindi.


Kwa mujibu wa taarifa hiyo, imetoa angalizo kwa mikoa mengine miwili ya Katavi na Rukwa kufuatia upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa kwa baadhi ya maeneo ya kusini mwa ukanda wa Ziwa Tanganyika.



“Athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na kuahirishwa kwa shughuli za baharini pamoja shughuli nyingine za bandari. Shughuli hizi ni pamoja na uvuvi na usafirishaji baharini,” taarifa hiyo ya TMA imeeleza.


Tahadhari hiyo inafanana na ile iliyotolewa na mamlaka hiyo Jumapili Juni 25, mwaka huu, ambapo utabiri ulionyesha kuwa mikoa tajwa ingeathiriwa na uwepo wa upepo mkali na mawimbi makubwa katika pwani ya bahari ya Hindi.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE