Viumbe 10 hatari ambao hupaswi kuwaamini

 Katika maisha yetu ya kila siku kuna mambo tunapitia lakini huenda kwa namna moja ama nyingine huwa hatufahamu mazingira halisi au athari za mambo hayo, Duniani kuna viumbe hai ambavy vingine tunaisghi navyo kirafiki na vingine vinahitaji akili kuweza kuishi navyo. Wapo wanyama ambao tumezoea kuwasikia au kuwaona lakini kutokana na kutokuwa na ukaribu nao ama kuzoeana nao tunaweza hisi ni kawaida kumbe ni hatari.



Kiumbe hai ni kitu kilicho hai kama vile binadamu, mnyama,mmea au bakteria, ambacho kina sifa ya kuzaliana, kukua, kula, kujongea, kuhisi, kupumua, kutoa taka za mwili na wapo ambao ni wapole na hatari lakini kuna wakali na hatari pia, kiasi leo hii nimekuandalia viumbe 10 ambavyo hutakiwi kuvichukulia kimasihara bali umakini.


1. Mbu, si kwamba wanaudhi pekee, lakini pia wanaeneza magonjwa hatari kama vile malaria, dungue na zika, magonjwa ambayo husababisha mamilioni ya vifo vya binadamu kila mwaka.


2. Mnyama wa Kiumbe cha Baharini kinajulikana kwa jina la Jellyfish – Sumu yao ina nguvu ya ajabu na inaweza kusababisha kifo kwa haraka, kwani ni hatari kwa mishipa ya moyo na kusababisha vifo vya Wanadamu.


3. Nyati, yeye anajulikana kwa kuwa na fujo na kusababisha vifo vya wawindaji zaidi, kuliko mnyama mwingine yeyote mkubwa wa porini na 4. ni Mamba mnyama anayeogopwa sana kwa mashambulizi mengi ya kushtukiza dhidi ya binadamu na mara nyingi kusababisha vifo.


5. Tembo, ingawa kwa kawaida ni wapole, wanaweza kuwa hatari sana wanapochokozwa na wanatajwa kusababisha vifo vingi vya binadamu kuliko mnyama mwingine mkubwa, na


6. Chura mwenye sumu ambaye huitwa jina la kitaalamu Poison Dat frog, licha ya umbo lao dogo, sumu yao ina nguvu sana na inaweza kusababisha kupooza au kifo kwa mtu aliyepata shambulio.


7. Mnyama bila shaka unamtambua hata kwa umbo akiitwa Dubu, yeye katika hali nadra, huweza kuwashambulia wanadamu na wanaweza kuwa hatari sana kwa sababu ya saizi na nguvu zao na


8. Nyuki, hawa ni hatari na muhimu pia kwa mambo yao ya asali na nta, ila anajulikana kwa kushambulia bila kuchoka, hujeruhi na hata kusababisha vifo.


9. Nzi, huku msumbufu sana na anasifika kwa kubeba na kusambaza vimelea vya magonjwa vinavyoweza kuwa ni vibaya na vyenye athari kwa wanadamu na wanyama, kuwa naye makini.


10. Fisi, kwanza huyu ni mlafi halafu hula nyama ya binadamu lakini kwa ujumla huwaogopa wanadamu.


Kwa hiyo, hawana hatari zaidi ila fisi wale wenye milia na fisi wengine wale wenye madoadoa wanaweza kumuua mtu na wakati mwingine wanaweza kumshambulia mwanadamu wakati mawindo yao ingawa matukio haya ni nadra kutokea hasa huko ulaya ila Afrika ni mwanzo mwisho na inasadikika wengine hutumika katika mambo yetu yale.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE