Vin Diesel afunguliwa kesi ya Unyanyasaji wa Kingono

 Nyota wa Filamu za Fast & Furious, Vin Diesel amefunguliwa mashtaka ya Unyanyasaji wa Kijinsia dhidi ya Asta Jonasson, Mwanamke aliyewahi kuwa Msaidizi wake mwaka 2010.



Mwanamke huyo amedai Septemba 2010 wakati wakirekodi vipande vya Filamu ya Fast Five aliitwa chumbani kwa Diesel akiwa peke yake ambapo alifanyiwa Ukatili wa Kingono ikiwemo Kushikwa Viungo vya Mwili bila ridhaa yake.


Ameongeza kuwa siku iliyofuata aliitwa na Samantha Vincent ambaye ni dada wa Diesel ambapo alitamkiwa kufukuzwa kazi. Hata hivyo Mwanasheria wa Diesel amekana tuhuma hizo na kudai Mwanamke ametunga uongo kwa maslahi binafsi.


Katika miaka ya hivi karibuni, Mastaa kadhaa wamejikuta katika matatizo tangu kuanza kwa harakati za kimataifa za #MeToo ambazo zimeshuhudia Watu maarufu wakiadhibiwa kwa Unyanyasaji na Ukatili dhidi ya Wanawake

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE