Tetemeko la ardhi laua watu 116 nchini china

 Watu 111 wameuawa na wengine 220 kujeruhiwa kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea Jumatatu usiku kaskazini-magharibi mwa Uchina, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.



Tetemeko hilo la kipimo cha 5.9 lilipiga mkoa wa Gansu mwendo wa saa sita usiku (16:00 GMT), na kuangusha majengo katika eneo hilo na mkoa wa Qinghai upande wa kusini.


Wafanyikazi wa dharura wanastahimili hali ya baridi kali kujaribu kusaidia watu katika eneo la mwinuko wa juu.


Tetemeko la pili lilipiga mkoa jirani wa Xinjiang saa chache baadaye Jumanne.


Uharibifu uliosababishwa na tetemeko hilo la kipimo cha 5.5 haujabainika.


Rais wa China Xi Jinping ameamuru juhudi za uokoaji katika Gansu, mojawapo ya mikoa maskini zaidi ya China.


Gansu iko kati ya nyanda za juu za Tibet na Loess na inapakana na Mongolia. Tetemeko la ardhi la Jumatatu usiku lilipiga mkoa unaojisimamia wa Linxia Hui, eneo la kiutawala la Waislamu wa Hui wa China.


Utafiti wa Jiolojia wa Marekani (USGS) ulisema ulikuwa na ukubwa wa 5.9 na kina cha 10km (maili sita).


Picha zilionyesha hospitali zikipokea wagonjwa, na waokoaji wakitafuta manusura kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka.


0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE