Somalia yafutiwa deni la Dola milioni 4.5

 

SERIKALI ya Somalia imefanya sherehe katika mji mkuu wa Mogadishu, baada ya IMF na Benki ya Dunia kutangaza msamaha wa deni la Dola bilioni 4.5.
Waziri Mkuu, Hamza Abdi Barre alisema unafuu huo ni sawa na kumuondolea kila Msomali deni la zaidi ya Dola 300″.

“Huu ni uthibitisho kwamba nchi yetu na watu wetu wana uwezo wa kifedha, na kuvutia wawekezaji kutoka nje, na hatuko tena na madeni.” alisema.

Msamaha huo pia unajumuisha msamaha wa wadai wengine wa kimataifa, wa nchi mbili na wa kibiashara.

Deni la nje la Somalia limeshuka kutoka 64% ya Pato la Taifa mwaka 2018 hadi chini ya asilimia 6 ya Pato la Taifa kufikia mwisho wa 2023.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE