Sasa ni New Amaan Sports Complex


ZANZIBAR: RAIS Rais Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi ameridhia ushauri wa kuubadili jina Uwanja wa Amaan na kuitwa “New Amaan Sports Complex” wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya uwanja huo uliofanyika Desemba 27, 2023.

Rais Mwinyi ameridhia ushauri huo uliotolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Damas Ndumbaro alipokua akitoa salamu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


“Kutokana na maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuufanya uwanja huu kuwa wa kisasa na wenye viwango vya kimataifa, mimi naomba niubadilishe jina uitwe New Amaan Stadium” alisema Dk. Ndumbaro.


Hafla ya Uzinduzi wa Uwanja huo ilipambwa na Burudani mbalimbali ikiwemo Muziki na mechi ya mpira wa miguu ya kirafiki baina Kilimanjaro Stars na “Zanzibar Heros ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE