Polisi yazuia mabasi saba Rukwa

 RUKWA: Jeshi la Polisi mkoani Rukwa kupitia kikosi cha usalama barabarani limeyazuia mabasi saba ya abiria kuendelea na safari za mikoani baada ya kukutwa na changamoto katika mifumo mbalimbali.



Hayo yamesemwa na mwanasheria wa kikosi cha usalama barabarani nchini Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP, Deusi Sokoni Desemba 28,2023 baada ya kuendelea na zoezi la ukaguzi wa magari, upimaji wa kilevi na utoaji elimu ya usalama barabarani kwa madereva na abiria katika stendi ya Katumba.


Aidha,amesema jumla ya mabasi 25 yamekaguliwa ambapo kati ya mabasi hayo saba yalikutwa na changamoto katika mifumo na hivyo kuzuiliwa kuendelea na safari.


Mabasi hayo yaliyozuiliwa ni, kampuni ya Ruchoro Express, Mbinga One express, Mwakamboja, MM8, Bubele trans, Mwasi express, Msigwa trans, yanayofanya safari ndefu kwenda mikoa mbalimbali nchini.


Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na mamlaka nyingine kama vile Mamlaka ya Udhibiti wa Vyombo vya Usafiri Aridhini (LATRA) imepewa mamlaka ya kuzuia chombo cha moto kuendelea na safari pindi linapofanya ukaguzi na kubaini changamoto ikiwemo ubovu au hitilafu katika mifumo ya chombo hicho alisema SSP Sokoni.


Kwa upande mwingine, Ofisa leseni kutoka mamlaka ya udhibiti wa vyombo vya usafiri aridhini (LATRA), Athumani Omary amesema wanafanya jitihada mbalimbali kuhakikisha abiria waliokuwa wamekata tiketi kwenye magari hayo wanapata usafiri mwingine ili waweze kuendelea na safari zao.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE