Polisi adaiwa kunyang’anywa gari na raia

 Kenya. Katika tukio lisilokuwa la kawaida watu wanne wamedaiwa kuliiba gari la Polisi kisha kutokomea nalo kusikojulikana nchini Kenya.

Inaelezwa watu hao walimvizia askari aliyekuwa na gari hiyo alipokuwa kituo cha mafuta kisha kumnyang’anya kwa nguvu.


Tovuti ya Tuko ya nchini humo imesema tukio hilo limetokea Jumamosi Desemba 23, 2023 mkabala na barabara ya Kisumu.


Taarifa zaidi zinasema mmoja ya watu hao alikuwa na bunduki aina ya AK47 ambapo askari huyo anayefanya kazi katika kituo cha Polisi cha Nyamasaria walimuibia pia na vitu vyake vingine.


“Kulingana na uchunguzi, mmoja wa watu hao alimwendea askari aliyekuwa na gari hiyo kabla ya wenzake watatu kujitokeza. Walimzidi nguvu na kumtoa kwenye gari na kumjeruhi kwenye mguu wake wa kulia.


“Kisha walitokomea na gari hilo. Aidha waliiba begi, redio ya polisi, daftari la polisi, pochi iliyokuwa na kadi ya ATM, kitambulisho, kadi ya bima ya afya na cheti cha kuteuliwa cha polisi,” imeeleza tovuti hiyo.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE