Muhimbili kuja na huduma ya kuhifadhi mbegu za uzazi

 

DAR ES SALAAM: Hospitali ya Taifa Muhimbili imepanga kuanza kutunza mayai kwa mtu asiye hitaji kupata mtoto kwa wakati husika na kutunza hadi kipindi anacho hitaji kupata mtoto.


Akizungumza wakati wa kuchangia Profesa Jay Foundation jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa, Mohamed Janabi amesema sio lazima watu waende nje kupandikiza kwani ndani ya hospitali hiyo wanapandikiza na kukutunzia mbegu hizo.


Amesema kuwa Hospitali ya Taifa Muhimbili inafanya jitihada kubwa kuboresha na kufanikisha matibabu mbalimbali kulingana na mahitaji yaliyopo kwa sasa nchini na sio hadi uende nje ya nchi.


“Sio lazima uende Uturuki kupandikiza mimba Muhimbili tunafanya na kama ukihitaji kuhifadhi mayai yako hutaki mtoto kwa sasa hadi hapo baadae tunakuhifadhia mayai yako hadi hapo baadae utakapokuwa tayari tutalikutanisha na kupata mtoto.”amesema Profesa Janabi.


Pia ameongeza kuwa Januari 2024, watafungiwa jengo la IVF ambapo watu hawatohitajika  kwenda Uturuki kupandikiza ujauzito.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE