Mahamaka yamwondoa Trump kugombea urais

 

MAHAKAMA ya Juu ya Colorado imeamua kuwa Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump hastahili kugombea urais wa taifa hilo kwasababu ya shambulio analohusishwa nalo la mwaka 2021 katika makao makuu ya Bunge Capitol Hill.


Uamuzi huo ni mara ya kwanza katika historia ya Marekani kwamba Kifungu cha 3 cha Marekebisho ya 14, ambacho kinamzuia mtu yeyote aliyejihusisha na uasi kutoka ofisi ya umma kimetumika kumuondoa mgombea urais.


“Mahakama nyingi zinashikilia kuwa Rais Trump amekataliwa kushika wadhifa wa Rais chini ya Sehemu ya 3 ya Marekebisho ya 14 ya Katiba ya Marekani,” mahakama kuu ya Colorado iliandika katika uamuzi wake.


“Kwa sababu ameondolewa, itakuwa ni kitendo kisicho sahihi chini ya Kanuni ya Uchaguzi kwa Katibu wa Jimbo la Colorado kumworodhesha kama mgombeaji kwenye kura ya mchujo ya urais.


Uamuzi huo ambao ulidhaniwa ungekatwa rufaa upande wa Trump ulilaaniwa mara moja na chama cha Republican.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE