Lee Sun-kyun: Muigizaji maarufu wa Korea Kusini amefariki

 

Muigizaji wa Korea Kusini Lee Sun-kyun, aliyepata umaarufu kwa uigizaji wake katika filamu ya Parasite iliyoshinda tuzo ya Oscar, amepatikana amefariki, mamlaka imethibitishia BBC.


Muigizaji huyo, 48, alipatikana akiwa amepoteza fahamu ndani ya gari katika moja ya bustani kuu za Seoul siku ya Jumatano.


Haijulikani ikiwa Lee alijiua, lakini polisi walisema walipokea ripoti kwamba aliondoka nyumbani baada ya kuandika barua.


Alikuwa chini ya uchunguzi kwa madai ya matumizi ya dawa za kulevya tangu Oktoba.


Katika filamu ya Parasite, Lee aliigiza kama mkuu wa familia tajiri ya Park ambayo inapenyezwa na watu wa familia maskini wanaojifanya kama watu wasiohusiana.


Tamthilia hiyo inayoangazia changamoto za kijamii ilishinda tuzo nne za Oscar, pamoja na picha bora zaidi.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE