Kinana azindua ujenzi wa Ofisi za CCM Bukombe

 

GEITA: MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amezindua ujenzi wa ofisi za CCM za pamoja na majengo ya kitega uchumi na kutaka maeneo mengine hususani katika ngazi ya kata na matawi, kuwa na ofisi za kisasa na kupongeza Bukombe kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama hicho 2020 – 2025 kwa vitendo.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Kinana amesema ilani ambayo imekua ikitolewa na CCM kuna sehemu inazungumza juu ya mambo yote, elimu, afya, miundombinu, utawala bora na kadhalika.



“Katika Ilani ya 2020 – 2025 sehemu ya 10, Ibara ya 246 imeweka mkazo kwenye shughuli zinazohusiana na Chama, nayo inasisitiza juu ya kusimamia maadili, nidhamu katika Chama, kusimamia mafunzo ya Chama na kukijenga katika misingi ya kuimarisha taasisi zake (jumuiya) kwa kujenga ofisi za Chama.

Amesema ni lazima Chama kujenga uwezo wa kujitegemea na Bukombe wameonyesha mfano kwa vitendo kuimarisha juhudi za kujitegemea hivyo alihimiza CCM kote nchini kuzingatie maagizo hayo ya Ilani kwamba ni lazima ibara hiyo itekelezwe kwa vitendo.



Awali Mkuu wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Said Nkumba ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi wa ofisi za Chama, amesema jengo la kitega uchumi lina nyumba ya wageni, mgahawa na samani zake, ofisi za kisasa na ukumbi wao una uwezo wa kuchukua watu 1000 kwa wakati mmoja, ujenzi wote ukigharumu zaidi ya Sh milioni 240.

“Hii ofisi tunayoizundua leo ni awamu ya pili ya ujenzi ikijumuisha ofisi ya Mwenyekiti wa CCM wilaya, Katibu, Makatibu wa jumuia zote, ofisi ya Mbunge, chumba cha Masjala, ofisi ya TEHAMA, ukumbi wa mkutano ya ya wajumbe wa halmashauri Kuu, duka na mgahawa wa kisasa,” amesema Nkumba



Amesema awamu ya kwanza ya ujenzi walijenga nyumba ya kupumzikia wageni yenye hadhi kubwa na hata kuweza kulaza wageni wa kitaifa na kwamba hivi karibuni Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda alilala hapo.

Kwa upande wa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Bukombe, . Dk Doto Biteko amemshukuru Makamu Mwenyekiti wa CCM (TZ) Bara, Komredi Abdulrahman Kinana kwa heshima aliyowapa CCM Bukombe ya kuzindua Majengo ya Ofisi.



Ameshukuru Wadau mbalimbali waliochangia katika ujenzi wa majengo hayo wakiwemo WanaCCM wenyewe ndani ya Wilaya ya Bukombe hasa Vijana wa CCM walioshiriki shughuli za ujenzi kwa kujitolea, wananchi wa makundi mbalimbali, baadhi ya Wabunge na viongozi wa Serikali.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE