Claudio Echeverri akaribia Man City

 

TETESI za usajili zinasema Manchester City inakaribia kumsajili kiungo Muajentina, Claudio Echeverri, 17,kutoka klabu ya River Plate katika dili ambalo huenda City ikamrejesha kinda huyo katika timu yake ya sasa hadi mwisho wa msimu wa Ligi Kuu England. (ESPN)


Arsenal ipo katika nafasi nzuri kumsajili beki wa Sporting Lisbon, 22, Goncalo Inacio, Januari 2024 huku mchezaji huyo mwenye kipengele cha kuachiwa cha pauni mil 66.3 pia akiwindwa na Liverpool.(A Bola – in Portuguese)


Tottenham ipo tayari kulipa pauni milioni 25 kumsajili kiungo wa kibelgiji Arthur Vermeeren, 18, kutoka klabu ya Royal Antwerp huku dili likihusisha kiasi kikubwa cha ada ya awali na makubaliano ya kumrejesha kwa mkopo kwa mabingwa hao wa Ubelgiji kwa muda wote uliobaki wa msimu.(Sun)


Manchester United inafikiria uhamisho wa mshambuliaji wa kidachi Joshua Zirkzee, 22, anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni mil 26 ambaye amepachika mabao saba katika michezo 17 msimu huu akiwa kikosi cha Bologna inayoshiriki Ligi Kuu Italia, Serie A.(Sport1 via Metro)


Paris Saint-Germain imekubaliana na timu ya Corinthians dili lenye thamani ya pauni milioni 17.34 kumsajili kiungo Mbrazil, Gabriel Moscardo, 18.(Fabrizio Romano)


Fowadi wa Brazil na Athletico Paranaense, Vitor Roque, 18, amekwenda Hispania kuanza mkataba wake Barcelona. Rogue alisaini mkataba wa miaka saba na mabingwa hao wa LaLiga Julai, 2023.(Fabrizio Romano)

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE