CCM Arusha wataka nidhamu, heshima

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Thomas Ole Sabaya amewataka wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Mkoa wa Arusha na wanachama wa wake kurejesha sura mpya, heshima, nidhamu na utaratibu ndani ya chama hicho.



Sabaya amesema hayo wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Arusha ambapo ameweka mkazo kwenye swala zima la nidhamu na kujali muda wa vikao


“Tunaomba ugonjwa huo wa muda uondoke naomba sana, niliahidi siku Ile kwamba tutakwenda kwa kukimbia kidogo ili tufufue uhai wa chama mpaka kule chini, tuonekane kwamba sio wale bali ni watu wengine wapya ambao tunajiandaa kwa ajili ya uchaguzi tukiwa mchakamchaka” alisema


Amesema upo ugonjwa kwa baadhi ya wajumbe kuja kwenye vikao aonekane na kuandika jina huku wakiwa wamekuja muda wanaojiskia wao na kutoka kabla ya kikao kuisha, Mazoea hayo ameomba yaondoke


“Sasa imekuja kufanya Nini?, sisi tumechaguliwa, unaaminika,watu wa chama na watu waserikali wanakuwa wewe ndio mwakilishi wao halafu unakuja unajionyesha halafu unaondoka, mazoea hayo naomba yaondoke.” alisema


Amesema kuwa kama umepewa dhamana basi heshimu dhamana hiyo, kama wewe ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya Mkoa wa Arusha, Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya ya Arusha, simama kwa nafasi yako na uonekane unashiriki na utoe maoni na ushiriki kikamilifu

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE