Aina 6 za ‘smartphones’ bora zaidi unazoweza kununua

 Hakuna simu moja inayoweza kuwa bora kwa watu wote. Kila mtu ana mapendeleo yake inapokuja suala la simu, wengine mbali na uwezo wa simu lakini pia huangalia kampuni husika au mifumo ya simu iwe ni iOS au Android.



Bila kujali simu unayoitaka, iwe ile ya gharama zaidi, au ya nafuu zaidi, orodha hii inaweza kukusaidia kufanya machaguo sahihi.


1. iPhone 14 iPhone 14 ya Apple ina kasi kama iPhone nyingine yoyote, yenye bei ghali zaidi ya Pro, na betri inadumu chaji karibu siku nzima. Kamera yake ina lenzi mbili na inatoa picha bora kwa kamera ya nyuma na hata ‘selfie’ na pia hurekodi video kwa ubora wa juu wa 4K.


Kama iPhones zote za kisasa, iPhone 14 inaweza kuhimili pale inapoingia maji hadi kwa hadi dakika 30.


2. iPhone SE (toleo la 3) iPhone SE (toleo la 3) ndio chaguo bora ikiwa unataka simu ndogo, na ni nafuu kuliko iPhone 14. Japokuwa ni simu nzuri lakini haina lenzi ya pili ya ultrawide ya iPhone 14 pamoja na mpangilio wa kamera wa ‘Night mode camera’, kwa hivyo kupata picha nzuri katika mazingira ya giza ni ngumu kidogo.


Ikiwa unatumia simu yako kucheza gemu, video na kadhalika, betri inaweza isidumu chaji lakini ikiwa si mtumiaji wa vitu hivyo, inaweza kudumu siku nzima bila kuchaji tena.


3. Google Pixel 7 Google Pixel 7 inatoa programu na kamera za ubora wa juu ambazo zimefanya simu zote za Google za Pixel kuwa bora. Simu hii ni toleo zuri la Google la Android 13, na linafanya kazi vizuri. Pixel 7 ina kamera mbili ambazo huchukua picha bora zaidi pengine kuliko simu nyingine yoyote ya Android.


4. Google Pixel 7 Pro Google Pixel 7 Pro ni toleo kubwa na bora zaidi la Pixel 7, yenye kioo kikubwa, inayojumuisha kioo cha inchi 6.7, OLED ya 1440p. Pia inajumuisha lenzi nzuri ya 5x katika kukuza (zoom) kamera ya nyuma.


Pixel 7 Pro ni mojawapo ya simu yenye utendaji wa haraka sana unayoweza kununua. Ina lenzi ya tatu yenye megapixel 48 ya nyuma yenye zoom ya 5x na inachukua picha bora zaidi.


5. OnePlus Nord N20 5G Ingawa OnePlus Nord N20 5G inagharimu nusu ya bei ya simu bora ya kisasa, kioo chake, uwezo wake na betri yake havina tofauti na simu hizo bira.


Hata hivyo ina camera yake inatajwa kuwa na changamoto hasa eneo ambalo halina mwanga wa kutosha.


6. Samsung Galaxy A03s Samsung Galaxy A03s ni simu nzuri yenye gharama nafuu na yenye programu nzuri. Simu hii inajumuisha mlango wa USB-C (badala ya muunganisho wa zamani wa USB ndogo ambao simu nyingi bado zinatumia). Ina kamera tatu za nyuma japokuwa ubora wake si wa kiwango cha juu.


Samsung imetoka kutangaza orodha yake kuu ya simu za Android 2023, Galaxy S23, S23+, na S23 Ultra, zitakazoanza kuuzwa hivi karibuni ambao wameahidi kamera za hali ya juu pamoja na lenzi ya megapixel 200.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE