Palestina yaendelea kuungwa mkono katika mashindano ya Kombe la Dunia, Qatar

 


Moja ya matukio yenye kuvutia katika mashindano ya Soka ya Kombe la Dunia huko Qatar ni kitendo cha watazamaji kutoka nchi mbalimbali kuiunga mkono Palestina mkabala wa utawala wa Kizayuni.


Katika Mashindano hayo dunia ya Soka mwaka huu wa 2022 huko Qatar, watazamaji wa nchi mbalimbali na hasa wa nchi za Kiarabu wamekataa kuhojiwa na vyombo vya habari na maripota wa Israel na wamekuwa wakionyesha uungaji mkono wao kwa Palestina wakati mechi mbalimbali zikifanyika. 


Watazamaji kutoka nchi mbalimbali walipeperusha bendera za Palestina katika mechi ya jana usiku iliyochezwa kati ya Croatia na Japan. Katika upande mwingine, mwanaharakati wa Kipalestina aligawa zawadi za lebo zinazovaliwa mkononi zenye picha ya Palestina kwa watazamaji kadhaa katika michuano hiyo na kupokelewa kwa wingi.  


Wakati huo huo, Abdullatif al Qanun Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Palestina (Hamas) amesema kuwa, kadhia ya Palestina ni suala kuu lililotawala mashindano hayo ya Kombe la Dunia huko Qatar na kusisitiza kuwa, suala la Palestina ni kadhia nyeti na kuu kwa Umma wa Kiislamu na iliyo katika mioyo ya mamilioni ya wapigania haki na ukombozi duniani.  



0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE