Sheria ya Kumiliki Laini MOJA Kwa Kila Mtandao Yaanza Leo



Sheria  iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni kuzuia kumiliki laini ya simu zaidi ya moja kwa mtandao mmoja wa simu imeanza kutumika leo, Julai 1, 2020.

Hata hivyo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa sheria hiyo haimzuii mtu kumiliki laini zaidi ya moja kwa mtandao mmoja, isipokuwa atalazimika kutolea ufafanuzi laini ya ziada. Lengo ni kudhibiti umiliki holela wa laini za simu na kudhibiti uhalifu.

Kifungu cha 18 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, sheria ya usajili wa laini za simu ya mwaka 2020 inaeleza kuwa mtu anatakiwa kumiliki laini moja ya simu kwa mtandao kwa ajili ya matumizi ya kupiga, kutuma jumbe na huduma za intaneti.

Sheria hiyo inaeleza kuwa mtu atakayemiliki laini zaidi ya moja kwa mtandao kinyume cha sheria atatozwa faini ya TZS 5 milioni au kifungo jela kwa miezi 12 au vyote kwa pamoja.

Na katika kila siku ambayo laini ya ziada ilitumika mhusika atalipa faini ya TZS 75,000 kwa siku.

Aidha, sheria hairuhusu kampuni kumiliki laini zaidi ya 30 ambazo zitatumika katika kupiga, kutuma jumbe au huduma ya intaneti. Endapo kampuni itakiuka sheria hiyo, itatozwa faini isiyopungua TZS 50 milioni pamoja na TZS 175,000 kwa kila siku ambayo laini za/ya ziada ilitumika.

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE