Nafasi za Masomo Chuo Cha Hombolo Kwa Mwaka 2020/2021

Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa (Hombolo) anakaribisha maombi ya kujiunga na masomo kwa mwaka 2020/2021 katika ngazi ya Astashahada (Certificate) na Stashahada (Diploma) kwenye fani zifuatazo:-

1. Utawala katika Serikali za Mitaa (Local Government Administration)
2. Usimamizi wa Rasilimali Watu (Human Resource Management)
3. Maendeleo ya Jamii (Community Development)
4. Uhasibu na Fedha katika Serikali za Mitaa (Local Government Accounting and Finance)
5. Utunzaji wa Kumbukumbu na Nyaraka (Records, Archives and Information Management)
6. Ununuzi na Ugavi (Procurement and Supply Management)

NAMNA YA KUOMBA KUJIUNGA NA MASOMO NI KAMA IFUATAVYO

1. Mwombaji wa “Astashahada ya Awali” yaani (Basic Technician Certificate – NTA Level 4)

Awe amepata angalau ufaulu wa “D” 4 katika masomo ya Kidato cha Nne (CSEE). Masomo ya Dini hayahusiki.

2. Mwombaji wa Astashahada yaani Technician Certificate -NTA Level 5

Awe amepata angalau ufaulu wa “Principal Pass” moja na “Subsidiary” katika mtihani wa Kidato cha Sita AU awe na Astashahada ya Awali yaani Basic Technician Certificate -NTA Level 4 toka Chuo chochote kilichosajiliwa na Serikali (na matokeo yake yawe yamepelekwa NACTE). Pia, awe amepata angalau ufaulu wa “D” 4 za Kidato cha Nne (CSEE). Masomo ya Dini hayahusiki.

3. Mwombaji wa Stashahada yaani Diploma- NTA Level 6

Awe na Astashahada yaani Technician Certificate-NTA Level 5) toka Chuo chochote kilichosajiliwa na Serikali. Pia, awe amepata angalau ufaulu wa “D” 4 za Kidato cha Nne (CSEE). Masomo ya Dini hayahusiki.

NAMNA YA KUOMBA:
Maombi yote yanafanywa kwa Njia ya Mtandao yaani Online Application System kupitia tovuti ya Chuo: www.lgti.ac.tz

MWISHO wa kupokea maombi ni tarehe 15 Septemba, 2020
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya chuo www.lgti.ac.tz au piga simu 026–2961101/0714684281/ 0755241010/ 0757488896

0 Comments

banner

Ahsante kwa kutembelea zotekali blog ili kuwa karibu nasi kila wakati Jiunge katika kurasa zetu zamitandao ya kijamii  facebook , Twitter, Instagram na Youtube  NI BUREE